Baraza la mawaziri Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Baraza la Mawaziri la Tanzania ni ngazi ya juu ya serikali au mkono wa utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mfumo wa mgawanyo wa madaraka.

Baraza hili linaundwa na rais, makamu wa rais, rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri wote. [1] Manaibu mawaziri si sehemu ya baraza. Mwanasheria Mkuu anashiriki katika mikutano ya baraza bila haki ya kupiga kura.

Mikutano ya baraza inaongozwa na Rais kama mwenyekiti, kama hayupo na Makamu wa Rais, na kama wote wawili hawapo na Waziri Mkuu.[2]

Serikali iliyopo ilitangazwa na John Magufuli, rais wa tano wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 mnamo tarehe 10 Desemba 2015. Isipokuwa nafasi 4 zilichelewa kutajwa majina hadi tarehe 23 Desemba, na hapo waliingia Jumanne Maghembe, Philip Mpango, Gerson Lwenge na Joyce Ndalichako. Siku hiyohiyo Makame Mbarawa alihamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Chama anachotoka Chama Cha Mapinduzi
Baraza la mawaziri la Tanzania: tangu Novemba 2015[3][4][5]
Picha Majukumu Jina
John Magufuli 2015.png Raisi
Amiri jeshi mkuu
Dr. John Magufuli
Samia Suluhu Hassan.jpg Makamu wa Rais Samia Suluhu
Ali Mohamed Shein, September 2014 (cropped).jpg Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein
Kassim Majaliwa.jpg Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
No image.svg Waziri wa Ofisi ya Raisi
TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
George Simbachawene
Angellah Kairuki.jpg Waziri wa Ofisi ya Raisi
TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
Angellah Kairuki
January Makamba 2012.jpg Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais
Masuala ya Muungano, Mazingira
January Makamba
No image.svg Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama
No image.svg Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba
No image.svg Wizara ya Katiba na Sheria Dr. Harrison Mwakyembe
Hussein Mwinyi.jpg Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi
No image.svg Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi Dr. Joyce Ndalichako
Wizara ya Nishati na Madini Sospeter Muhongo
No image.svg Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango
Augustine Mahiga (cropped).jpg Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga
No image.svg Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
No image.svg Wizara ya Mambo ya Ndani Charles Kitwanga
Charles Mwijage.jpg Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage
No image.svg Wizara wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye
William Lukuvi cropped.png Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
No image.svg Wizara ya Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe
Makame Mbarawa IAEA.png Wizara ya Maji na Umwagiliaji Gerson Lwenge
No image.svg Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa (alihamishwa kuoka kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji tar. 23.Desemba 2015)
(anahudhuria mikutano ya baraza la mawaziri bila kupiga kura
No image.svg Mwanasheria Mkuu wa Tanzania George Masaju

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Cabinet of Tanzania. tanzania.go.tz (May 2012). Iliwekwa mnamo May 2012.
  2. Katiba ya Tanzania, fungu 54
  3. Baraza la Mawaziri. Ikulu (10 December 2015).
  4. "Magufuli releases long awaited cabinet", 10 December 2015. 
  5. Kigezo:Cite tweet

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Wizara za Serikali ya Tanzania Orodha_ya_Mawaziri_Wakuu_wa_Tanzania